UKARABATI KAITABA WAIPELEKA LIGI KUU CCM KIRUMBA MWANZA‏

UAMUZI wa Shirikisho la Soka (TFF) wa kuufanyia  ukarabati uwanja wa Kaitaba  wa mkoani Kagera, umetoa fursa kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kushuhudia baadhi ya mechi za Ligi Kuu.

Uwanja wa Kaitaba ambao umekuwa ukilalamikiwa na timu mbalimbali kutokana na ubovu,umefungwa kupisha ukarabati utakaowezesha uwekewe nyasi bandia.

Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa  wa Kagera,watakutana na uongozi wa klabu ya Kagera Sugar ili kufahamu watatumia uwanja upi kwenye mechi zao za nyumbani za Ligi Kuu.

Kagera italazimika kuhamisha na kucheza nje ya mkoa huo mechi zake zote za Ligi Kuu hadi hapo uwanja huo wa Kaitaba utakapokamilika .

TFF tayari ilishatangaza kuwa mechi kati ya Kagera na Mbeya City,itachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza,uwanja ambao ni mzuri na uko jirani na Mkoa wa Kagera.

Kuhamishiwa kwa mechi za Ligi Kuu kwenye uwanja wa CCM Kirumba ni faraja kwa wapenzi,washabiki na wadau wa soka hapa,baada ya kuikosa kwa muda mrefu,tangu Toto ishuke daraja msumu uliopita.

Kaitaba ni miongoni mwa viwanja ambayo vimekuwa vilalamikiwa kutokana na kuwa na mabonde na miinuko ,hivyo kuwekewa nyasi bandia kutaondoa  malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya timu zilizokuwa zikiutumia kucheza na Kagera Sugar .

.
Mbali na Kaitaba,mwingine ambao uko kwenye ukarabati wa kuwekewa nyasi bandia ni uwanja mkongwe wa Nyamagana wa Jiji la Mwanza, ambao uko katika hatua za mwisho ili kuwekewa zuria la nyasi hizo.

Mwisho

Post a Comment

أحدث أقدم