Mlipuko
wa kisiri wa unyanyasaji wa kingono katika hospitali za Uingereza
umegunduliwa huku takwimu mpya zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600
yaliripotiwa kwa polisi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.
Kumbukumbu
zilizopatikana na gazeti la The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa
habari zinaonyesha ongezeko la asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa
kingono kwa kutumia nguvu katika hospitali tangu mwaka 2011.Ripoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za kibinafsi,na vituo vyengine vya afya.
Lakini viongozi wa mashtaka wanasema kuwa hadi asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji haviripotiwi swala linaloonyesha kwamba takwimu za ukweli huenda ziko juu zaidi.
Post a Comment