Kesho mwisho tuzo za filamu za Tafa

ZILE tuzo kubwa zinazoandaliwa na shirikisho la filamu Tanzania, lipo katika hatua za mwisho kabisa baada ya kukamilika taratibu zote, hivyo kwa wale washiriki wanakumbushwa kuwakilisha fomu za ushiriki wa tuzo hizo.
“kwa wale wote waliochukua FOMU kwa ajili ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha TUZO za Filamu Tanzania (TAFA), mnapaswa kuzingati tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu hizo kwa Katibu Mkuu wa TAFF kama ilivyoelekezwa, siku ya mwisho ni IJUMAA ya tarehe 2 JANUARI 2015”,anasema Bishop.
Tarehe rasmi kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo itatajwa baada ya ukusanyaji na mchakato kukamilika wakati wowote kutoka shirikisho, usipoteze nafasi hiyo adimu kwa kushiriki na kujipima kupitia kazi yako utakayowakilisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post