Walimu 18 kutoka Kiruna, Sweden wawasili
leo kwa ajili ya kuanza kazi ya ufundishaji. Walimu hao watakaokuwa
nchini kwa kipindi cha mienzi minne watasomesha ujasiriamali,
kiingereza, kompyuta na demokrasia kwa watoto wa kike wa Makunduchi.
Kuja kwao nchini kunafuatia makubaliano baina ya wadi za Makunduchi na
Manispaa ya Kiruna. Ujumbe wa wadi za Makunduchi ulifanya ziara ya
kikazi ya wiki moja mwanzoni mwa Disemba mwaka jana.


Afisa tawala mstaafu wa wilaya ya
Kusini, ndugu Abdallah Ali Kombo akionekana kuwa na furaha wakati
akimpokea ndugu Simon, mmoja ya walimu watakaofundisha watoto wa kike
huko Makunduchi

إرسال تعليق