Wanachama, Viongozi wa chama kipya cha ACT Watwangana Ngumi ndani ya Ofisi ya Msajili

Vurugu zimetokea jana kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania kukutana ana kwa ana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kikao cha usuluhishi.
 
Baada ya kukutana kwa makundi hayo, ghafla walitokea vijana wanaodaiwa kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia Katibu Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson Mwigamba.
 
Vurugu hizo zimetokea ikiwa ni siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kumsimamisha uongozi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
Mwigamba alidai vijana hao wamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia vurugu baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.
 
“Limbu alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la Kinondoni pamoja na kina Mahona.
 
“Wakati tunatoka kikaoni nikawa pale nje nasubiri gari linichukue, akaja Gerald huku akishika shati langu akidai ananidai shilingi milioni moja na lazima nimlipe pale pale, nilishangaa sana na hapo ndiyo nikajua kuna kitu Limbu amefanya ili wale vijana wanivuruge na baadaye nikasirike na kuonekana nimepigana,” alisema Mwigamba

Post a Comment

أحدث أقدم