WATU
wanne wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha
basi la Abiria la Hajees likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam na lori
katika eneo la Mandera Mkoani Pwani leo asubuhi.
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, SACP
Ulrich Matei amesema kuwa abiria hao waliruka kutoka katika basi hilo
kuhofia ajali ya kugongana na lori lililokuwa likitokea mbele ya basi
hilo na ndipo walipoangukia barabarani na kupelekea vifo vyao, baada ya
dereva wa basi kutoka nje ya barabara.
Aidha
Kamanda Matei amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wa Chanzo cha ajali
hiyo wanamshikilia dereva wa lori hilo ambalo lilisababisha vifo vya
abiria hao walioruka kutoka katika basi la Hajees
إرسال تعليق