Washukiwa
wa mauaji ya wachora vibonzo nchini Ufaransa, wanadaiwa kufanya wizi
katika kituo cha mafuta Kaskazini mwa Ufaransa huku wakiwa mbioni
kutoroka polisi.
Inaarifiwa washukiwa hao wawili ambao ni ndugu,
waliiba chakula na petroli huku wakifyatua risasi hewani karibu na eneo
la Villers-Cotterets.Watu nchini ufaransa walikaa kimya kwa dakika moja kwa heshima ya watu 12 waliouawa na watu wenye silaha walipovamia gazeti moja la vibonzo la Charlie Hebdo siku ya Jumatano
Wakati huohuo, msako mkubwa wa polisi unaendelea Kaskazini Mashariki mwa Paris, ambako washukiwa waliovamia ofisi za jarida la Charlie Heblo, wanasemekana wamejificha.
Huku polisi nchini ufaransa wakiendelea kuwatafuta wanaume hao kumeripotiwa kutokea shambulizi lengini mjini Paris
Afisa wa kike wa polisi aliuawa wakati mwanamume mmoja alipompiga risasi eneo moja kulikotokea ajali ya barabarani.
Waziri mkuu nchini Ufaransa Manuel Valls anasema kuwa washukiwa hao (Said Kouachi na Cherif Kouachi) walikuwa wakifahamika kwa mashirika ya kijasusi.
Akiongea baada ya mkutano na rais wa ufaransa, mkuu wa chama cha upinzani cha UMP na raisi wa zamani Nicolas Sarkozy wamesema kuwa shambulizi hilo ni la kinyama


إرسال تعليق