Dar/mikoani. Watoto 174 wamezaliwa katika hospitali mbalimbali
za mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Manyara na Mara wakati wa mkesha wa
kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Wakati watoto wakizaliwa, wengine wawili walifariki dunia muda mfupi baadaye.
Ofisa Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala, Rehema Kessy alisema jana kuwa watoto 23 waliozaliwa hapo, 15 ni kiume.
Kessy alisema watoto wote wapo katika hali nzuri na hakuna mzazi alijifungua kwa upasuaji.
“Wazazi wengine wameshaondoa hospitali...hawa
waliobaki watapewa ruhusa mchana (jana) ili wakasherekea mwaka mpya na
vichanga vyao,” alisema Rehema.
Katika Hospitali ya Amana, watoto 21 walizaliwa huku 11 wakiwa wa kike.
Muuguzi wa wa hospitali hiyo, Rose Mkondola
alisema: “Kati ya watoto 21, wa kike wawili walifariki baada ya kuzaliwa
na wakati wowote kuanzia sasa tutawapa ruhusa hawa wazazi na watoto
kwani hali zao zinaendelea vizuri,” alisema Rose.
Mmoja wa wazazi hao Halima Issa, mkazi wa Kiwalani
alimshukuru Mungu kwa kujifungua salama, huku mtoto wake akiwa
anaendelea vizuri.
Ofisa Muuguzi wa Zamu Hospitali ya Temeke,
Rolester Kinunda alisema watoto 19 walizaliwa kwenye mkesha huo na kati
yao watoto wa kike ni tisa.
Alisema mmoja alizaliwa kwa upasuaji baada ya uchunguzi kubaini kuwa alikuwa mkubwa.
Alisema mzazi huyo na mwanaye wapo chini uangalizi huku wazazi wengine wakipewa ruhusa kutokana na afya zao kuimarika.
Mkoani Morogoro watoto 17 walizaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Post a Comment