Zaidi ya watu 50 wamenusurika kifo katika ajali ya moto wakati
wakijalibu kupora saruji kwenye gari la mizigo lililopasuka tairi moja
ya mbele na kusababisha mlipuko mkubwa wa moto kwenye tenki la kuhifadhi
mafuta baada ya kushindwa kuzima moto uliotekete za gari hilo sehem ya
mbele katika kijiji cha nterungwe wilaya ya ngara mkoani kagera.
Gari hilo lililokuwa likitoka mkoa wa tanga kuelekea nchi ya
burundi kupitia kabanga wilaya ya ngara a mkoani kagera limepata ajali
hiyo majira ya saa moja na dakika 30 za usiku ambapo dereva wa gari hilo
ameiambia ITV kuwa baada ya gari kupata hitilafu ya kuwaka moto ameomba
msaada kwa wananchi ambao wamejaribu kuzima gari kwa mchanga na maji
bila mafanikio ndipo likaibuka kundi la watu kupora saruji baada ya
jeshi la polisi kuchelewa kufika kwenye eneo la tukio.
Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi linawashikilia watu kumi kwa
tuhuma ya wizi na gari tatu zilizokamatwa zikiwa na saruji za wizi
ambapo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa
wilaya ya ngara Bw.Costantine Kanyasu amezungumza na ITV kwa njia ya
simu akiwataka wananchi kuacha tabia ya kupora vitu kwenye ajali kwani
kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.
Wilaya ya ngara iliyopo pembezoni mwa mkoa wa kagera inapakana na
nchi ya burundi na rwanda inakabiliwa na changamoto mbalinbali za
miundombinu ikiwemo ukosefu wa gari ya kuzima moto hali inayohatarisha
maisha ya watu pindi kunapotokea majanga ya moto.
- ITV

إرسال تعليق