WATU
wawili wakazi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi wameuawa kikatili ambapo
mmoja amecharangwa kwa mapanga na mwili wake kukatwa vipande vipande
kisha kuzikwa shambani kwake na mwingine kuchinjwa na watu wanaodaiwa
kuwa wa familia yake.
Inadaiwa kutokana na hofu waliyokuwa nayo watoto hao walisita kurejea nyumbani kumsaidia baba yao mzazi.
Kamanda Kidavashari amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia mtoto wa marehemu Kanedeku Giti (26) akihusishwa na kifo hicho cha baba yake mzazi
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kutokea
kwa mauaji hayo na kusema aliyekatwa vipande ni Minza Mwanalushinga (26)
mkazi wa kitongoji cha Vilolo, katika kijiji cha Manga, kata ya Kibaoni
wilayani Mlele.
Mwingine
kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari ametambuliwa kuwa ni Giti Mawiti (53)
mkazi wa kijiji cha Tupindo - Minyoso wilayani Mlele ambaye inadaiwa
alikutwa amechinjwa.
Akisimulia
tukio hilo Kamanda Kidavashari alisema tukio la kwanza lilitokea
Januari 15, mwaka huu, saa moja jioni katika kitongoji cha Vilolo ambapo
Mwanalushinga anadaiwa aliondoka alfajiri kwenda kuchota maji umbali wa
kilomita moja na wakati akirejea nyumbani kwake alivamiwa na watu
wasiojulikana na kumburuza hadi shambani kwake kisha wakamcharanga kwa
mapanga na kumkata vipande vipande na kuvifukia shambani kwake.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo, tayari Jeshi la Polisi mkoani humo
linawashikilia watu wawili akiwemo mume wa marehemu, Kimbulu Joseph na
jirani yake Joseph Abel kwa uchunguzi zaidi.
Katika
mkasa mwingine ambao unadaiwa kutokea Januari 16, mwaka huu, saa tatu
usiku katika kitongoji cha Tupido, marehemu Giti Mawiti (53) alikuwa
nyumbani kwake akisumbuliwa na tumbo ndipo alipowaamsha watoto wake
Kanedeku Giti (26), Kabula Giti (21) na Nyanzobe Giti (16) ili
wamchemshie maji anywee dawa huku yeye akiwa amejilaza barazani.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari ghafla alitokea mtu akiwa na tochi yenye
mwanga mkali na kuwamulika machoni ambapo watoto wote hao walikimbia na
kumwacha baba yao ambapo muda mfupi baadaye wakiwa mafichoni walimsikia
baba yao akipiga kelele za kuomba msaada.
Kamanda Kidavashari amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia mtoto wa marehemu Kanedeku Giti (26) akihusishwa na kifo hicho cha baba yake mzazi

إرسال تعليق