Vijana 510 wanaodaiwa kujihusisha na vitenda vya kihalifu chini
ya kundi maarufu la ‘panya road’ wamekamatwa na jeshi la Polisi Kanda
Maalum jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.
Watuhumiwa hao wamekatwa katika mikoa ya kipolisi
ya Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo jeshi la polisi limefanya msako
mkali kuweza kuwabaini lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi nchini.
Kamishna wa Polisi Suleiman Kova ametoa wito kwa
wazazi wa watoto hao kutofika kwenye vituo ambavyo wamehifadhiwa mpaka
watakapo kamilisha uchunguzi wao dhidi yao.
Kamanda Kova amesema kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa maeneo mbalimbali ikiwamo kwenye vijiwe huku wengine
wakifuatwa katika nyumba wanazoishi baada ya polisi kupata taarifa za
kinterenjensia.
“Tulipowapekua watuhumiwa hawa tuliwakuta na
vichocheo kadhaa vya uhalifu ambavyo ni puli za bangi 113, kete zake
676, na misokoto 294 na vinginevyo, pia kati yao wapo wakubwa zao watatu
ambao ndiyo vinara wa mgogoro”.amesema Kova
Amesema operesheni ya kupambana na ‘Panya Road’
itakuwa endelevu hadi pale jina hilo ambalo limekuwa gumzo jijini
litakapotoka kabisa masikioni mwa watu.
Aidha kamanda Kova amesema jeshi la polisi kwa
sasa limejipanga katika kutoa mafunzo maalum kupitia wenyeviti wa
Serikali za Mitaa kwa mikoa yote ya kipolisi ili kukabiliana na vitendo
hivyo vya uhalifu.
“Ni ukweli usiopingika kuwa vijana wanao fanya
vitendo hivi wanafamika kwa wananchi wa eneo husika lakini wanakuwa
wasiri kufichua uovu huo hivyo kupitia mafunzo haya yatasaidia kuondoa
tatizo hili,” amesema Kamishna.
Januari 2 mwaka huu hali ya taharuki, hofu na
wasiwasi mkubwa iliwakumba wakazi wa jiji hilo kwa saa mbili baada ya
kundi maarufu la waporaji la Panya Road, kuvamia mitaa mbalimbali na
kupora mali
Post a Comment