Kijana aliyeamua kujiweka wazi juu ya chaguo lake
Pameibuka
hasira kali miongoni mwa jamii ya Wagoa nchini India,wakati ambapo
serikali ilipoamua kuweka bayana kuwa kutakuwa na vituo vya kuwaponya
wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja.
Waziri wa michezo na
mahusiano ya vijana Ramesh Tawadkar ameeleza kuwa tiba itatolewa kwa
wanawake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja,wanaume wanaoshiriki
mapenzi ya jinsi amoja,wanaobadili jinsia zao,na wapenda jinsia zote
mbili lengo ni kuwafanya warejee katika utu wao wa awali.
Baada ya
tamko hilo jamii ya Goa ilihamishia mjadala katika mitandao ya kijamii
huku walio wengi wakimpinga Tawadkar kwa matamshi yake ya kushtusha.
Mnamo
mwaka 2013,mahakama kuu nchini India iliubadili uamuzi wa mahakama ya
mwanzo kwa kuitupilia mbali sheria ya mkoloni kutoka Uingereza iliyodumu
kwa takribani miaka 153,na kutoa tamko la kwamba nchini humo mapenzi ya
jinsi moja ni kosa la jinai,na kuleta mjadala mkubwa ulimwenguni na
huku wengine wakiuita uamuzi huo kuwa ni wa kufedhehesha.
Kwa
muujibu wa kifungu cha 377 cha sheria za nchini India,mapenzi ya jinsi
moja ni makosa makubwa kinyume na asili na ukikutwa na hatia hukumu yake
ni miaka kumi jela.
Mwandishi wa BBC mjini Delhi anaeleza kuwa
hata hivyo sheria hiyo haijaanza kufanya kazi kwa uzito unaostahili na
badala yake polisi wamekuwa wakiitumia kuwanyanyasia wapenzi wa jinsi
moja.
Nchini India wahafidhina wa kale ,ushiriki katika mapenzi ya
jinsi moja ni mwiko na jamii ina mtazamo tofauti juu ya mahusiano hayo
na huyachukulia kuwa ni haramu na tamko la waziri Tawadkar ni sawa na
kuruhusu mahusiano hayo na kukinza fikra za wahafidhina.
Naye
alisikika akisema tutawarejesha wapenzi wa jinis moja katika hali zao za
awali.tutakuwa na kituo kwa ajili yao kama ambavyo wanaojaribu kujitoa
katika ulevi wa kupindukia walivyo na kituo chao,tutawapatia mafunzo na
kuwapa dawa pia,alisema waziri huyo mwenye dhamana,wakati akiwasilisha
ripoti inayohusiana na vijana .
Makundi mengine ya vijana walengwa
juu ya masuala ya vijana wahalifu,wanaotumia dawa za
kulevya,waliotelekezwa na wahamiaji,vijana walioathiriwa na mazingira
ripoti ihusianayo na vijana endapo itatoka itakuwa imeangazia changamoto
zinazowakabili na namna ya kukabiliana nayo hasa suala la mapenzi ya
jinsi moja.
Mtandao wa Twitter tangu mwanzoni mwa wiki hii umegubigwa na ujumbe mkali wenye kumkosoa waziri huyo kuhusiana na tamko lake.

إرسال تعليق