Wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wao katika Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji wameapishwa jana kuanza kutumikia wananchi kulingana na nafasi zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, walitaka serikali kuangalia suala la kulipa mishahara kila mwezi kwa wenyeviti na wajumbe hao.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mnazi Mmoja, kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma Ujiji,
Nuru Bashange alisema nafasi ya wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao
itambulike rasmi kikatiba na walipwe mishahara kama wanavyolipwa wabunge
na madiwani.
Bashange
alisema wenyeviti wa maitaa na wajumbe wao wamekuwa na jukumu kubwa la
kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo
yao.
Alisema
imefika wakati sasa wa serikali wa kuona umuhimu wa kuwapatia mafao ya
kutosha kila mwezi viongozi hao badala ya posho ya Sh elfu kumi kwa
mwezi inayolipwa sasa.
Mwenyekiti
huyo wa Mtaa alisema hata kama madiwani hawalipwi mishahara lakini
kiwango cha posho wanacholipwa hakina uwiano na kiwango wanacholipwa
wenyeviti wa mitaa.
Kwa
mujibu wake, ni wakati wa kufanya maboresho kwenye malipo kuwatia moyo
wenyeviti hao katika kusimamia utendaji na utekelezaji wa mipango ya
maendeleo bila kufuata vishawishi.
Pamoja
na madai hayo kwa serikali wenyeviti hao wameahidi kutumia nafasi zao
katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo kama ambavyo nia na
dhamira yao iliwatumia na kuamua kugombea nafasi hizo.

إرسال تعليق