Pc
Damiani Christiani wa polisi mkoa wa Singida,akitumia chombo maalum
kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wa zoezi la
kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha
Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa
wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom
Tanzania.
PC.Abdalah
Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo
maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati zoezi
la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha
Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa
wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom
Tanzania.
Mrakibu
msaidizi wa Jeshi la polisi (ACP) mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma
makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam,Abel
Swai,akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa
likitokea Dodoma kwenda Arusha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo
watagundua dereva mlevi au akiendesha gari vibaya,ili hatua za haraka
ziweze kuchukuliwa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya"Wait to
send"inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia
vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
MRAKIBU
msaidizi wa polisi makao makuu kitengo cha elimu kwa umma usalama
barabarani (trafiki) ACP,Abel Swai,amewataka madereva wa mabasi nchini,
kuhakikisha wanakuwa watanashati kwa kuvaa nguo zinazolingana na unyeti
wa kazi yao,ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kukubalika na
kuaminika na wateja wao (abiria.
ACP
Swai metoa wito huo jana wakati akisimamia zoezi la kupima ulevi
madereva wa mabasi na kuhakikisha sheria,taratibu na kanuni za usalama
barabarani kama zinatekelezwa ipasavyo.Zoezi hilo linaloendeshwa na
Jeshi la polisi kwa ushirikiano na Baraza la Taifa la usalama barabarani
na Vodacom Tanzania,lilifanyika katika kituo kikuu cha mabasi mjini
Singida.
Alisema
kwamba wapo baadhi ya madereva wa mabasi licha ya kutofaa sare ya
kampuni zao akiwa barabarani,wanavaa nguo ambazo hazifafani na heshima
ya kazi anayoifanya, kitendo ambacho baadhi ya abiria kupunguza imani
kwake kwa kudhani sio dereva makini.
"Kazi
ya udereva wa mabasi ina heshima ya kipekee.Kwa hiyo ni lazima dereva
pamoja na kutekeleza kazi yake kikamilifu,pia anapaswa awe nadhifu kwa
mavazi yake na vitendo vyake vingi vikubalike mbele ya jamii",alifafanua
zaidi ACP Swai.
Kuhusu
zoezi lao,mratibu huyo msaidizi,alisema sambamba na zoezi la kudumu la
kupima madereva walevi,pia wamekuwa wakikangua madereva watumiaji wa
vyombo vya moto,watembea kwa miguu na wasukuma matoroli kama
wanazingatia kikamilifu sheria zote za usalama barabarani bila shuruti.
"Lengo
letu ni kuwakumbusha madereva,abiria na wananchi kwa ujumla wajibu wao
wawapo barabarani.Abiria kama wanagundua gari wanalosafiria ni
mbovu,wamecheleweshwa,dereva ni mlezi au makosa yo yote ya jinai,atoe
taarifa haraka kwa jeshi la polisi.Hali kadhalika madereva watimize
wajibu wao kwa mujibu wa sheria.Wakati wote wazingatie au waheshimu
alama na mistari iliyowekwa barabarani"alisema.
Alisema
endapo kila Mtanzania atatambua anatakiwa afanye nini ili kuokoa maisha
ya mwezake,ajali ya barabarani zinazopotesha maisha ya watu na mali
zao,zitapungua kwa kiasi mkikubwa.
ACP
Swai ametumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuacha kutumia pombe
wakati wakiwa barabarani kwa madai kwamba zinasabaisha wakose umakini na
kunza kutoa maamuzi ambayo ni hatari kwao na wateja wao.Pia amesema ni
marufuku mabasi ya masafa marefu kuwa na dereva mmoja,ni lazima wawe
wawili.
Katika
zoezi la kupima madereva watumiaji wa pombe wakiwa barabarani,
lililofanyika mjini hapa jana,madereva wawili wa nje ya mkoa
huu,waligundulika kutumia pombe na wanashikiliwa na jeshi la polisi
mjini hapa.
إرسال تعليق