1 na 2 Kutoka Kwa Lady jaydee, Afunguka Mazito instagram, Kwanini sifanyi collabo na wasanii wa kike, Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio

1.  Kwanini sifanyi collabo na wasanii wa kike? 🙉🙉🙉🙉 Jibu :
Nimewahi kufanya na wasanii mbali mbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia. 👍👍👍👍👍
1.Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Kaysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba nae Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali
Na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu
Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio.
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo
Need i say more?


A photo posted by Judith Wambura Mbibo (@jidejaydee) on



2. Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio
Na mpango wa kupatana nao :

JIBU :
Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha.
Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha
Otherwise hakuna miujiza
Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .
Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote
Hakuna binadamu asie kosea
Ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.
Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua .

Je! Hili jibu limejitosheleza?
Naamini hata nyinyi mmewahi kutofautiana na watu wenu wa karibu.
Kukubali kosa ndio mpango



Post a Comment

Previous Post Next Post