AMANDA AANIKA SIRI NZITO YA KUTOWAPENDA WANAUME

MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi amefunguka na kueleza siri nzito kuwa hawapendi wanaume kutokana na kufiwa na mchumba wake muda mfupi baada ya kuzungumza naye miaka…iliyopita.

Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi.
Akipiga stori na gazeti hili, Amanda alisema stori ya mwanaume ambaye alikuwa ni mchanganyiko wa Mgiriki na Mbongo aliyejulikana kwa jina la Alan kila akiikumbuka huwa inamuumiza  moyoni kwani ni mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati.
“Huwa naumia sana nikimkumbuka Alan mchumba ambaye alikuwa ameshajitambulisha kwetu lakini akafariki kwa ajali nusu saa baada ya kuzungumza naye kwenye simu akiwa Ugiriki huku akiniachia ujauzito wa miezi mitano lakini ilipofika miezi saba mtoto alifia tumboni. “Tangu hapo sipendi wanaume na sijawahi kumpata mwanaume mwenye upendo wa dhati kama huyo,” alisema Amanda.

Post a Comment

أحدث أقدم