Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua
sera mpya ya elimu nchini na kusisitiza kuwa serikali itaweka sawa
viwango vya utozaji wa ada kwa shule binafsi nchini, Askofu wa Dayosisi
ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.
Fedrick Shoo, amesema serikali inaweza kufanikisha mpango huo, lakini
hatma ya kukua au kuporomoka kwa sekta hiyo ipo mikononi mwa wadau.
Alisema suala hilo linapaswa kuwashirikisha wadau wote, kwa kuwa
wadau hao, wamekuwa kitovu cha elimu kwa miaka mingi, hata kama serikali
imejipanga kufanya utafiti wa kina kukabiliana na changamoto hiyo,
kabla ya kupanga na kutangaza viwango elekezi vya utozaji wa ada.
Dk. Shoo alikuwa akizungumza juzi katika Shule ya Sekondari ya
Mtakuja iliyopo Kata ya, Wilaya ya Moshi wakati wa uzinduzi wa masomo
kwa njia ya ‘tablets’, mpango ambao KKKT imeeleza kwamba unalenga
kuchochea wanafunzi kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi.
“Sera mpya ya elimu iliyozinduliwa, naamini itamaliza udhaifu
uliokuwa ukipigiwa kelele na wadau kwa miaka mingi sasa, ikiwamo suala
la mitaala, lakini kama taifa, tuanze kuthamini juhudi za marafiki wa
elimu wanaotuunga mkono,” alisema.
Alisema Taasisi ya Opportunity Education Foundation (OEF)ya
Marekani, imeamua kuwekeza katika mikoa 10 ya Tanzania, ikivutiamasomo
ya Sayansi.
Alisema mpango huo wa kuvutia wanafunzi kupenda zaidi masomo ya
Hisabati, Biolojia aio, Kemia, Kiingereza, Jiografia na Historia,
unalenga kuongeza kiwango cha ufaulu na idadi ya wataalam katika fani
hizo.
Mkuu wa Shule hiyo, Emanuel Lyatuu, aliwaeleza wadau wa elimu
mkoani kuwa masomo hayo yatafundishwa kwa njia ya elektroniki tofauti na
ilivyozoeleka ubaoni na kwamba wanafunzi watalazimika kufanya mitihani
yao ya muhula kwa njia ya mtandao. Taasisi hiyo ya Marekani imeipatia
tablets 65.
Ofisa Mipango wa OEF, Juliana Bwire, alizitaja shule 10 za
Sekondari zilizochaguliwa nchini kuingia katika mpango wa majaribio wa
miaka miwili kuwa ni Mtakuja (Kilimanjaro), Ilboru wanaume na Peace
House (Arusha), Bwiru wanaume (Mwanza), Mzumbe (Morogoro) na Wama
(Rufiji).
Nyingine ni Josaya wanawake (Bukoba), Msalato wanawake (Dodoma),
Fidel Castro (Pemba) na Shule ya Sekondari ya Mchepuo wa Kiingereza ya
Loleti (Zanzibar).
Mwakilishi Mkazi wa Taasisi hiyo nchini, Mchungaji Martin Russel,
alisema kuwa OEF imekuja na teknolojia mpya iliyoboreshwa zaidi duniani
ya kuvutia masomo ya Sayansi kwa kutumia video 733 ambazo zinatumika
kukuza uelewa wa mwanafunzi darasani.
إرسال تعليق