Basi la Kidia lapata ajali laua

BASI la Kidia lenye namba za usajili T663 AXL lililokuwa linatoka dar kwenda Mwanza limekugonga lori lenye namba za usajili T 496 CFG na trela lenye namba za usajili T576 AZX Scania na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine 45 kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea leo saa 7.05  kwenye kijiji cha Vikon je wilayani Chamwino.Waliokufa katika ajali hiyo ambayo roli lilikuwa linatoka Dodoma kwenda dare s salaam ni dereva wa lori, Fadhili Said (36) na utingo wa basi, Chogo Chigunda.
Kamanda Misime alisema ajali hilo ilitokea wakati dereva wa basi la Kidia, Adam Robert (34) alipokuwa akilifuata gari lilokuwa likilipita gari la mbele yake.

Post a Comment

أحدث أقدم