Daz Baba Afunguka, Stereo na muigizaji Niva Nao pia Wamo, Wasikilize Hapa Kapitia 255 ya Leo

Nimekuwekea  255 ya leo February 09, kutoka kwenye show ya XXL na story ya kwanza kusikika inamhusu mwanamziki mkongwe Daz Baba ambaye amezungumzia ishu ya familia yake  na kusema kuwa kwa sasa anaishi peke yake na anahangaika kwa ajili ya kuwatengenezea maisha watoto wake wawili ambao wanasoma, amekuwa akiwatembelea mara kwa mara huku akipewa support na mzazi mwenzake japo hawako pamoja.
532096_363335017105221_492332328_n 
Muigizaji  aliyefanya vizuri katika movie kadhaa pamoja na tamthilia ya Jumba la Dhahabu, Niva amesema kuwa hivi sasa ameamua kuingia rasmi kwenye muziki ambao aliwahi kuufanya kabla hajaingia kwenye uigizaji lakini kipindi hicho muziki ulimtesa sana akiwa na ndugu yake ambaye waliwahi kufanya wote kazi kwa producer Enrico.
stereo 2 
Story ya mwisho kusikika kwenye 255 inahusu tukio la kusikitisha lililotokea siku ya Jumamosi inayohusu familia ya watu sita waliofariki kwa ajali ya moto Ukonga ambao ni ndugu wa msanii  wa Stereo.
Stereo amesema taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha moto huo kilisababishwa na hitilafu ya umeme, watu waliokuwa wakitoa msaada walijaribu kuwapigia simu Askari wa Zimamoto lakini walichelewa kufika na kushindwa kutoa msaada wowote, mazishi ya wanafamilia hao yatafanyika  kesho huko Ukonga Banana.
Bonyeza play kuweza kusikilia 255 ya leo hapa.

Post a Comment

أحدث أقدم