Dar es salaam. Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk
Harison Mwakyembe amesema Tanzania haitazuia magari ya Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki au Nchi nyingine kuingia katika viwanja
vyake vya ndege kuleta au kuchukua Watalii wanaopitia katika viwanja
hivyo na kwenda katika nchi zao.
Akizungumza na waandishi wa hahabari jijini Dar es
Salaam leo, Dk. Mwakyembe amesema serikali ya Kenya wameenda kinyume
na mkataba wa mwaka 1985 kwa kuvihusisha viwanja vya ndege kuwa sehemu
ya vivutio vya utalii jambo lililopelekea kukatazwa kwa magari ya
Kitalii yaliyo sajiliwa Tanzania kuingia uwanja wa ndege wa Jomo
Kenyata.
Dk Mwakyembe amesema Waziri wa Maliasili na
Utalii tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii
Kenya katikati ya mwezi Januari ,2015 lengo la kikao hicho ilikuwa ni
kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kukatazwa kwa maghari katika uwanja wa
ndege wa Kenya
“Suala la kurekebisha mkataba ulioingizwa na nchi
hizi mbili kwa hiari miaka 30 iliyopita si jepesi, linahitaja mjadala
mrefu utakaohusisha taasisi mbalimbali. Hata hivyo vyombo husika
vinafanyia kazi suala hilo,amesema Dk Mwakyembe
Amesema Tanzania itachukua hatua ya kuwafahamisha
Watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea vivutio vya kitalii vya
Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepusha kadhia na
gharama zisizo za lazima.
Dk Mwakyembe aliongeza kuwa suala la Magari ya
Tanzania kukatazwa kuingia kwenye kiwanja cha Jomo Kenyatta nchini Kenya
halitakiwi kabisa kurudisha mahusiano mema miongoni mwa nchi hizi
mbili.
إرسال تعليق