Wiki
hii Lady Jaydee amewapa nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali naye
kuyajibu kupitia akaunti yake ya Instagram. Ameulizwa maswali mengi, na
miongoni mwa maswali hayo ni la kuhusu ndoa yake na mtangazaji wa Radio
E-FM Gadner G. Habash.
Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram.
Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?
JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha
Kwanini umeachana/umemuacha mume?
JIBU :
Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha,
amani na upendo. .. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo , sikuwa
tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha
jamii.
Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume? JIBU :
Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshma zaidi kuishi na mume
asie na heshma, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati
mi niko jukwaani naimba.
Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini . Ukiachilia mbali vipigo.
Kutembea
na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao. …..niliwahi mkuta
anawashika mapaja na akakiri kosa. bado kupigana na kuwatusi wateja pia.
Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.
Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?
JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi
Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.
Kwanini usirudiane na mumeo?
JIBU :
Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpk kuamua
kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. … When i say
never, I mean Never.
Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?
JIBU : Nilidhani
angebadikika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe
tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka
mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha
mtu mzima.
Uliwezaje kuondoka?
JIBU :
Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri
kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima km kweli
ntaweza ku move on?
Niliporudi
Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpk muda huu nnapo type na ku post
haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu
ya kuaga. Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.
Post a Comment