MWANADADA
kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi amefunguka na kueleza
siri nzito kuwa hawapendi wanaume kutokana na kufiwa na mchumba wake
muda mfupi baada ya kuzungumza naye miaka…iliyopita.
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi.
Akipiga stori na gazeti hili, Amanda alisema stori ya mwanaume ambaye
alikuwa ni mchanganyiko wa Mgiriki na Mbongo aliyejulikana kwa jina la
Alan kila akiikumbuka huwa inamuumiza moyoni kwani ni mwanaume
aliyekuwa na mapenzi ya dhati.
“Huwa naumia sana nikimkumbuka Alan mchumba ambaye alikuwa
ameshajitambulisha kwetu lakini akafariki kwa ajali nusu saa baada ya
kuzungumza naye kwenye simu akiwa Ugiriki huku akiniachia ujauzito wa
miezi mitano lakini ilipofika miezi saba mtoto alifia tumboni. “Tangu
hapo sipendi wanaume na sijawahi kumpata mwanaume mwenye upendo wa dhati
kama huyo,” alisema Amanda.
Post a Comment