Godzilla wa Sengerema amuibukia Godzilla( @King_Zillah ) wa Salasala kwa madai ya kuibiwa jina

Picha ni msanii wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa anayemshutumu Godzilla wa Salasala kamwibia jina lake.
Na Daniel Makaka, Sengerema
Msanii wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa, mwenye makazi yake kijiji cha Bupandwa Kata ya Bupandwa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ameibuka na kusema kuwa aliibiwa jina hilo  na msanii maarufu wa Hip Hop, kutoka Salasala,  Golden Mbunda  “ Godzilla”  ambaye msanii huyo anajiita hivyo.
Akizungumza na mwandishi wetu kutoka Kanda ya Ziwa, Alisema awali Godfrey ambaye alikuwa akiishi  Mbezi Kimara mtaa wa Tanesco jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa  msanii huyo wa Salasala, Godzilla, aliiba jina lake hilo hali iliyompelekea usumbufu mkubwa katika sanaa yake.
“Mimi ndie msanii mwenye jina hili tokea miaka mingi. Lakini nikashangaa msanii mwingine anajiita Godzilla, hivyo kutokana na kuwa ni msanii mwenye malengo nimeamua kuja na jina jipya la ‘God One’.  na kuachana na jina ambalo aliibiwa hapo awali” alieleza God One, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaoenda kwa jina la ‘Mimba’.
GodZilla_full
Msanii maarufu wa Hip Hop, kutoka Salasala, Golden Mbunda “Godzilla” 
Hata hivyo ameomba wapenzi na mashabiki wake wamtambue kwa jina la God One ambapo licha ya kutamba na kibao hicho cha ‘Mimba’,  pia anajiandaa kutoa wimbo mwingine.
Hata hivyo modewjiblog, ilipomtafuta Msanii wa Salasala, Godzilla  kuhusiana na kuiba jina la Godzilla wa Kanda ya Ziwa, kwa upande wake, alionesha kushangazwa na jambo hilo ambapo  alipuuza habari hizo na kukata simu.
Tasnia ya sanaa nchini  kwa miaka mingi, wasanii na watu mbalimbali wamekuwa wakiibuka kwa madai ya kuibiwa kazi zao hizo za sanaa ikiwemo nyimbo, majina na style ambapo wameishia kulalamika huku wakikosa haki zao.
Timu ya mtandao huu wa modewjiblog, itaendelea kufuatilkia sakata hili mpaka mwisho wake.
IMG_0861
 Msanii wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa anayemshutumu Godzilla wa Salasala kamwibia jina lake.

Post a Comment

Previous Post Next Post