Picha
ni msanii wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa
anayemshutumu Godzilla wa Salasala kamwibia jina lake.
Na Daniel Makaka, Sengerema
Msanii
wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa, mwenye
makazi yake kijiji cha Bupandwa Kata ya Bupandwa wilayani Sengerema
Mkoani Mwanza ameibuka na kusema kuwa aliibiwa jina hilo na msanii
maarufu wa Hip Hop, kutoka Salasala, Golden Mbunda “ Godzilla” ambaye
msanii huyo anajiita hivyo.
Akizungumza
na mwandishi wetu kutoka Kanda ya Ziwa, Alisema awali Godfrey ambaye
alikuwa akiishi Mbezi Kimara mtaa wa Tanesco jijini Dar es Salaam,
ameibuka na kusema kuwa msanii huyo wa Salasala, Godzilla, aliiba jina
lake hilo hali iliyompelekea usumbufu mkubwa katika sanaa yake.
“Mimi
ndie msanii mwenye jina hili tokea miaka mingi. Lakini nikashangaa
msanii mwingine anajiita Godzilla, hivyo kutokana na kuwa ni msanii
mwenye malengo nimeamua kuja na jina jipya la ‘God One’. na kuachana na
jina ambalo aliibiwa hapo awali” alieleza God One, ambaye kwa sasa
anatamba na wimbo wake unaoenda kwa jina la ‘Mimba’.
Msanii maarufu wa Hip Hop, kutoka Salasala, Golden Mbunda “Godzilla”
Hata
hivyo ameomba wapenzi na mashabiki wake wamtambue kwa jina la God One
ambapo licha ya kutamba na kibao hicho cha ‘Mimba’, pia anajiandaa
kutoa wimbo mwingine.
Hata hivyo modewjiblog,
ilipomtafuta Msanii wa Salasala, Godzilla kuhusiana na kuiba jina la
Godzilla wa Kanda ya Ziwa, kwa upande wake, alionesha kushangazwa na
jambo hilo ambapo alipuuza habari hizo na kukata simu.
Tasnia
ya sanaa nchini kwa miaka mingi, wasanii na watu mbalimbali wamekuwa
wakiibuka kwa madai ya kuibiwa kazi zao hizo za sanaa ikiwemo nyimbo,
majina na style ambapo wameishia kulalamika huku wakikosa haki zao.
Timu ya mtandao huu wa modewjiblog, itaendelea kufuatilkia sakata hili mpaka mwisho wake.
Msanii wa nyimbo za Bongo flava, Godfrey Ally kutoka Kanda ya Ziwa anayemshutumu Godzilla wa Salasala kamwibia jina lake.
إرسال تعليق