Kama wewe ni mtumiaji au mtembeleaji wa mitandao ya kijamii [na sijui
 nani hatumii hii mitandao siku hizi kwa njia moja au nyingine] bila 
shaka leo umeona habari inayozunguka kuashiria kwamba jikoni inapikwa 
collabo kati ya msanii wa Tanzania Ali Kiba na yule wa Marekani, Chris Brown.
Nilipoziona habari hizi, binafsi nilifurahi kwani naamini kwenye 
mafanikio ya sanaa na wasanii wa kitanzania katika kufika mbali zaidi 
kwa minajili ya kuitangaza Tanzania, utamaduni wake [ikiwemo 
muziki,sanaa nk] na hata kuwatangaza watu wake. Kila mtu mwenye akili 
timamu bila shaka anawaombea na kuwatakia kila la kheri wasanii wetu 
waendelee kutaka kutimiza ndoto zao za kufika mbele zaidi. Isitoshe Ali 
Kiba aliwahi kufika anga za mbali kiasi cha kushirikiana na artists 
wengine wakubwa barani Afrika na hata Marekani. Bila shaka unakumbuka 
project ya One8 iliyomkutanisha Ali na mkongwe wa R&B R.Kelly.
Lakini wakati naendelea kuisoma habari yenyewe, ghafla tabasamu langu
 likaanza kupungua kabla halijapotea kabisa. BBC Swahili? Mbona kwenye 
tovuti yao rasmi ya BBCSwahili.com habari hii siioni?  Tangu lini BBC Swahili wakatumia “blog”? Na mbona mengi yanayoelezewa hayaendani na kile ninachokifahamu? Tangu lini Ali Kiba yupo chini ya Samsung? Mbona VIP Beats ni wauzaji wa beats na sio watu wa habari? Kweli BBC wawe na site ambayo ina posts 2 tu? Mmmh
Nikaona nijiridhishe kwa kuwasiliana na uongozi au management ya Ali 
Kiba. Ndipo nilipoupata UKWELI kwamba habari hiyo haina ukweli hata 
kidogo na kwamba hakuna kitu kama hicho kwa hivi sasa. Naam. Tuendelee. 
Hili si la kweli! [Ila kama nilivyosema hapo juu, lingekuwa la 
kweli…sote tungelifurahia au sio?]


Was that guy taking beats from Lazy Rida?
ردحذفإرسال تعليق