Matukio ya wanawake kukataa tamaa ya kuolewa na kujichukua sheria
mkononi sasa yameanza kushika kasi, tumesikia stori ya mwanamke kuamua
kuvaa shela la harusi na kukatiza nalo mitaani huku mwigine naye akiamua
kujioa mwenyewe wote sababu ikiwa moja kukataa tamaa ya kuolewa.
Habari nyingine ni kwamba msichana huyu raia wa Uingereza ameamua
kukatisha maisha yake kwa kujinyonga baada ya kufikisha miaka 29 huku
akiwa hana dalili yoyote ya kuoelewa wala kupata mtoto.
Rachel Gow aliamua kuchukua uamuzi huo ikiwa ni
miezi miwili imebaki kabla ya kuhitimisha miaka 30,na kifo chake
kimetokana na kukata tamaa ya kuolewa pamoja na kifo cha mama yake mzazi
ambacho kilimwongezea uchungu.
إرسال تعليق