MSANII
wa muziki kutoka TMK Family, Chege Chigunda amezua gumzo la aina yake
baada ya picha akiwa amevaa kitambaa cheusi kwenye mkono wake wakati
akipafomu jukwaani kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kuwa ni
hirizi.
Wasanii wa muziki kutoka TMK Family, Chege Chigunda wakishambulia jukwaa.
Picha hizo zilipigwa kwenye Tamasha la PSPF mkoani Dodoma
lililofanyika February 20 Mwaka huu ambapo Chege na Temba waliokuwa
wakipafomu jukwaani zilimuonesha Chege akiwa na fulana iliyokatwa
mikononi yenye maandishi mekundu na meusi huku mkono wake wa kushoto
ukiwa na kitambaa hicho.
Picha hiyo iliyotupiwa kwenye mitandao iliwashangaza watu waliodai
kuwa ni mambo ya kiswahili huku wakikitaja kitambaa hicho kama hirizi,
lakini wengine walidai kuwa kuna maelezo ya ziada kutoka kwa msanii huyo
kwa kuwa kama angevaa hirizi asingevaa fulana aliyoikata mikono.
Mwandishi wetu alizungumza na Chege ambaye alikanusha taarifa za
kuvaa hirizi na kudai kuwa hicho ni kitambaa cheusi ambacho wasanii wote
waliokuwepo Dodoma siku hiyo walishauriana kukivaa wakiwa na maana ya
kuguswa na msiba wa mwanamuziki mwenzao Mez B aliyefariki mapema siku
hiyo.
“ Halafu nyinyi mwandishi (tusi) sana huwezi kusema mimi nimevaa
hirizi wakati nilivaa kitambaa cheusi, wa hujui kuwa siku ile Mez B
alikuwa amefariki. Acheni u(tusi) wenu,” aliongea kwa lugha chafu na
kuongeza; “Subirini niongee na Shigongo sasa hivi,” alisema na kukata
simu huku Temba, ambaye alikuwa naye pichani, akiwa hana kitambaa hicho.
Post a Comment