Moja ya Jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya mtaa wa Libya na Mosque likiendelea kuwaka moto huku Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiangalia namna ya kuudhibiti moto huo.
Gari la Zimamoto la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam likiwasili eneo la tukio.
Kazi ikiendelea.
Mara mabomba kadhaa yakazidiwa na nguvu ya maji na kupasuka,lakini haikuwa tatizo kwani ilikuwe mingine kibao ya rizevu.
Kazi ikiendelea.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova
akijaribu kufanya mawasiliano na vyombo mbali mbali vya zimamoto.
Mamia
ya wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio la Moto Mkubwa uliozuka
mapema leo kwenye majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
yaliopo kwenye makutano ya mtaa wa Libya na Mosque kuteketeza eneo lote
la juu la Majengo hayo.Chanzo cha moto huo hakikuweza fahamika mpaka
tunaingia mitamboni japo tetesi zinaeneleza kwamba ni hitilafu ya uemem.
Kazi zilisimama kwa watu wengine wa maeneo ya jirani na tukio hilo.
Vikosi vya Zimamoto toka makampuni mbali mbali vilijipanga vyema kabisa kukabiliana na tukio hilo.
Kikosi cha Zimamoto cha Faya kikiendeleza uhodari wake wa kuzima moto ulioenea kila pembe ya majengo hayo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeswad Nkongo akizungumza na
vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.
Mwanalibeneke
Othman Michuzi (kushoto) akiwa katika mavazi maalum pamoja na Maafisa
wa Kikosi Zimamoto wakati wa zoezi la uzimaji moto huo mchana wa leo
jijini Dar.
Sasa
tumemaliza kazi na shukrani za dhati kwa maafisa wa kikosi cha Zimamoto
waliokuwa bega kwa bega na wanahabari kuhakikisha uzimaji wa moto huo
unakwenda vema.
- Picha Na Matukio- Michuzi
إرسال تعليق