Waongo
wengi huwa hawakumbuki walichokisema hapo kabla, hivyo huleta uongo
mwingine mpya kabisa bila kujua. Hivyo hivyo hutokea pia pale ambapo
unaamua kudanganya kwenye CV yako wakati wa kuomba au kutafuta kazi, na
wengi wanaona ni kawaida tu ilimradi wapate kazi.
Kumbuka
kuwa kazi hiyo inahitaji mtu mwenye vigezo husika, hivyo unapodanganya
kwamba una taaluma fulani au ujuzi fulani ambao moja kwa moja haupo
kwenye vyeti vyako au kwenye vitu ulivyojifunza itakupa shida kama ni
kitu ambacho mwajiri anakuajiri ili atumie ujuzi huo.
Watu
wengi hudanganya kwenye ujuzi wao na uwezo wao wa kiutendaji
Inawezekana una vyeti stahiki kabisa na unaweza kupata kazi hiyo bali
kama unafanyiwa usaili usiongee vitu ambavyo huwezi kuvifanya kwani
baadaye utawajibika katika hivyo. Kuna watu wengi hujikuta wanalazimika
kuachia ngazi kwa sababu walidanganya kwenye CV zao na hivyo kujikuta
hawawezi kazi, hivyo inawabidi waacha kazi kwa visingizio tofauti
tofauti.
Ikigundulika
umedanganya waajiri wengi hawataweza kukupa kazi kama umepitia kwa
taasisi zinazoajiri kwa niaba ya makampuni husika, kwani CV yako na
jina lako wataambiana kwenye taasisi hizo. Utasota kutafuta kazi
kwasababu ya ujinga wako. Unatakiwa uwe mkweli na ujue nini unafanya
kila wakati na kwa kila sehemu unayoomba kazi.
Kama
umedanganya kwenye CV yako inamaanisha hata kazini utakuwa mdanganyifu
na hilo likigundulika,hautakuwa mtu wa kuaminiwa na mwajiri hivyo kosa
dogo la uaminifu litakusababishia kufukuzwa kazi.
Maamuzi
ni yako hivyo chukua maamuzi madhubuti kuhakikisha kile unachoandika
kwenye CV yako ni ukweli kuhusu wewe na ni kile unachoweza kukifanya.
Ukigundulika
mara nyingi unatakiwa kufukuzwa kazi, kwani wewe ni mtu hatari katika
nyanja hiyo, inaweza kusababisha kupewa majukumu ambayo yakahatarisha
biashara au kampuni na kusababisha matatizo makubwa hivyo kiuhalisia
hauhitajiki hata kidogo. Mahali pengine unaweza kupandishwa kizimbani
kwa kosa hilo, hivyo uwe mwangalifu usiingie tamaa harafu ukafanya
maamuzi ambayo yatahribu taaluma yako.
إرسال تعليق