JIKE DUME LAZUA KIZAAZAA


Dume zima ovyoo! Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja amezua kizaazaa ukumbini baada ya kutinga akiwa amevalia nguo za kike na kuonekana kama mwanamke.


Mwanaume huyo tata (kulia) akikata mauno.
Mwanaume huyo aliyepachikwa jina la Jike Dume hilo alinaswa na Amani katika Ukumbi wa Flamingo ulipo Magomeni, Dar, wiki iliyopita wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’ ilipokuwa ikitoa burudani ambapo jamaa huyo alikuwa amevaa sketi na blauzi ya kike huku kichwani akiwa ametupia wigi.
Katika hali ya kushangaza, mwanaume huyo alionesha hana chembe ya aibu kwani alikuwa akikata mauno mbele ya jukwaa na wakati mwingine aliwakatia viuno wanaume wenzake.“Duh! Kweli dunia imefika ukingoni jamani, hebu mwangalie yule mwanaume amevaa nguo za kike utadhani mwanamke halafu anawakatikia mauno wanaume wenzake bila hata aibu,” alisikika mmoja wa waudhuriaji wa shoo hiyo.
Baada ya kukwepa kunaswa na kamera yetu mara kadhaa baadaye ilifanikiwa kumnasa akikata mauno kwenye steji huku akirembua macho yaliyochorwa wanja na mdomo uliopakwa lipstiki kama mwanamke.

Post a Comment

أحدث أقدم