WATU watano
wamekufa na wengine zaidi ya 170 wamelazwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu ulioukumba mkoa Kigoma.
Akizungumza mjini Kigoma leo Mganga Mkuu wa mkoa kigoma,Leonald Subi amesema kuwa Manispaa ya Kigoma Ujiji imeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo na kwamba tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kukabiliana na hali hiyo.
Subi alisema kuwa tangu mwezi Januari mwaka huu ugonjwa huo ulioanza kuripotiwa kwenye wilaya ya Kasulu na manispaa ya Kigoma Ujiji watu 175 walikuwa wamekumbwa na ugonjwa huo katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku wilaya ya Kasulu ikiwa na wagonjwa wanane.
Alisema kuwa kwa manispaa ya kigoma Ujiji eneo lililoathiriwa ni kata ya kibirizi ambako sehemu kubwa ya wagonjwa waliougua na kufariki walitoka huko na kwamba tayari kambi ya wagonjwa wa kipindu pindu imefunguliwa kwenye kituo cha afya cha Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Post a Comment