KIWANDA CHA 21ST CENTURY CHAPIGWA KUFULI


Majitaka yenye Sumu hatarishi kutoka Kiwanda cha Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni Morogoro ambapo Wanachi hutumia maji ya Mto huo kwa matumizi ya nyumbani. (Picha na OMR)

Majitaka yenye Sumu hatarishi kutoka Kiwanda cha Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni Morogoro ambapo Wanachi hutumia maji ya Mto huo kwa matumizi ya nyumbani. (Picha na OMR)
Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya kfungwa shughuli za uzalishaji katika Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatiwa na kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .
Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.
Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka kiwandani hapo haina uwezo wa kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.

Post a Comment

أحدث أقدم