KOCHA wa Simba, Goran Kopunovic, alifanya uamuzi mgumu juzi
Jumapili katika mchezo na Polisi Morogoro kwa kuamua kumweka benchi
straika namba moja wa timu hiyo, Danny Sserunkuma na kumwanzisha Ibrahim
Ajibu jambo ambalo anasema alikuwa sahihi kabisa.
Kocha huyo mwenye mbwembwe nyingi, alisema hawezi
kumpanga mchezaji kwa kuangalia anatoka nchi gani ama alifanya nini
katika mechi ya mwezi uliopita, bali anaangalia mahitaji ya timu kwa
wakati huo na umakini wa mchezaji husika.
Uamuzi wa Kopunovic kumuweka benchi Sserunkuma
umefanyika ikiwa ni wiki moja na nusu pekee tangu straika huyo
alipoifungia Simba mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT
Ruvu.
Mserbia huyo aliongeza kuwa Sserunkuma anatakiwa
kufunga kila mechi na si kushangilia mabao aliyofunga katika mechi
zilizopita huku akisifu kiwango kilichoonyeshwa na Ajibu katika mechi
yao hiyo ya juzi.
Ajibu na Elius Maguli walifunga bao moja kila mmoja na kuipatia Simba ushindi wa mabao 2-0 ugenini.
“Naangalia mafanikio ya timu zaidi na si mchezaji
mmoja mmoja, nilichofanya ni kwa manufaa ya timu na nitaendelea
kuwapanga wachezaji kutokana na uwezo na si eneo analotoka.
“Dan (Sserunkuma) alifanya makosa mengi katika
mechi ya Coastal Union, alikosa nafasi tatu hadi nne za wazi hivyo
nikalazimika kubadili mfumo na kumchezesha Ajibu,” alisema kocha huyo wa
zamani wa Polisi Rwanda.
AZIONYA AZAM, YANGA
Baada ya kikosi chake kupaa hadi nafasi ya nne
katika msimamo wa ligi na kupunguza wigo wa pointi na vinara wa ligi
Azam na Yanga kutoka pointi nane hadi tano, Kopunovic amezitahadharisha
timu hizo kuwa zikae chonjo kwani anakuja.
Alisema bado ana mechi dhidi ya Azam na Yanga
ambazo kama akishinda ataweza kupunguza wigo huo na kuwakaribia kabisa
wapinzani wake hao.
“Bado tuna nafasi, wigo wa pointi kati yetu, Azam
na Yanga si mpana sana, kumbuka bado ligi imebakisha mechi 12 na kati ya
hizo zipo ambazo tutacheza nao, ni lazima tushinde mechi hizo ili
kuwakaribia ama kuwafikia,” alisema Kopunovic mwenye umri wa miaka 48.
IVO KUREJEA UWANJANI JUMATANO
Post a Comment