Chama cha kutetea abiria nchini Tanzania CHAKUA leo
wameibuka na kuzitaka mamlaka husika kushusha nauli za mabasi ya mikoani na
daladala mara moja kwa kile walichosema kuwa ni kutokana na kushuka kwa bei ya
mafuta duniani.EXAUD MTEI ANASIMULIA ZAID
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es
salaam mwenyekiti wa chama hicho HASSAN
MCHANJAMA amesema kuwa mafuta yakipanda anayenufaika ni mmiliki wa vyombo vya
usafiri kwa kupandisha nauli hivyo mafuta yakishuka hawana budi kushusha bei za
nauli ili kumpunguzia mzigo mtumiaji ambaye ni mwananchi wa kawaida.
Amesema kuwa imekuwa ikitokea mafuta yakipanda kidogo
tu wamiliki wa vyombo vya usafiri wamekuwa wakikimbilia kupandisha nauli mara
moja lakini yanaposhuka wamekuwa wakikaa kimya kana kwamba hawajui kama yameshuka
jambo ambalo ameliita ni kumkandamiza mwananchi wa kawaida ambaye ndiye abiria.
Amesma kuwa tayari chama cha kutetea abiria wamekwisha
waandikia barua SUMATRA kwa lengo hilo na kuitaka iitishe mkutano na wadau ili
wajadili jambo hilo lakini SUMATRA wamekuwa kimya jambo ambalo linaonyesha bado
hawana nia njema kwa mtanzania wa kawaida.
Amesema kuwa CHAKUA inataka bei zote zipungue kwa asilimia 25 ambapo nauli za dala dala ambazo kwa sasa ni shilingi mia 400 ipungue na kufikia shilingi 300 na kwa upande wa mabasi yaendeyo mikoani mambo yawe hivyo hivyo ambapo mfano mabasi ambayo nauli ni shilingi elfu 40 bei hiyo ipungue na kufikia elfu 30 huku pia bei za usafiri wa majini zipungue kwa asilimia 25.
Amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa
wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa watapata hasara endepo watashusha bei ya
nauli jambo ambalo amesema kuwa sio kweli na hakuna hasara yoyote watakayopata kwani
ipo faida kubwa sana wanayopata kwani mafuta duniani imeshuka.
إرسال تعليق