Madabida: Sina kambi, wanaohangaika hawajielewi

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema yeye hayumo kwenye  kambi yoyote ya  wanaharakati wanaowania urais ndani ya CCM na kusisitiza kuwa   kambi yake ni moja tu CCM.
Madabida aliitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa  wananchi wa Mtaa wa Kijichi  kwa kukipa kura chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji 2014.
“Madai hayo siyo ya kweli, mimi sipo katika kambi yoyote,  kambi yangu moja tu Chama cha Mapinduzi.” Madabida ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwashukuru wananchi hao wa mtaa wa kijichi kwa kukipa kula chama cha CCM kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtaa huo, Ramadhan Kiula. 
Akizungumza na wananchi hao, Madabida alisema nchi yetu inachangamoto nyingi ikiwamo za kiuchumi, kisiasa na kijamii  na kwamba CCM inajitahidi kukabiliana nazo  hivyo aliwataka wananchi wasifanye wasifanye makosa katika uchaguzi ujao kwa sababu  sumu haionjwi.
Madabida amesema kuhusu Katiba  inayopendekezwa  mengi  yamesemwa na yanaendelea kusemwa lakini ni kweli ajenda yake ni ya CCM ambayo ipo madarakani, siyo ya wapinzani  ila Katiba siyo ya CCM ni ya wananchi.
“Rasimu ya pili ya  Katiba haikuwa Msahafu ama Biblia, ndiyo maanda kulikuwepo na bunge maalum la Katiba ambapo lengo lilikuwa ni kuijadili, kuichambua na inapobidi kubadilishwa na lilifanya hivyo  kwa kufanya mabadiliko ya maboresho katika mambo mapya kwa asilimia 15 kati ya 100.”Alisema Madabida.
Kuhusu uchaguzi wa uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji 2014, Madabida alikiri kuwa kulikuwepo na ushindani mkubwa  na akaongeza kuwa kuna  mambo mengi wamejifunza  ambayo yatatusaidia  katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk Faustine Ngugulile aliwataka wananchi hao kuisoma katika inayopendekezwa kwa kina na katiba ya zamani ili waweze kufahamu wanapiga kura ya nini.
Dk Ndugulile alisema wao kama CCM wanasema Katiba hiyo inayopendekezwa inatosha na kuwataka wananchi wasije kurubuniwa  ifikapo Aprili 30,2015 wajitokeze kuipigia kura.
Pia aliwataka wananchi kujitokeza katika kujiandikisha kwa kuwa wasipofanya hivyo kula ya maoni n ahata uchaguzi mkuu hawatashiriki kwa sababu vitambulisho vya vya zamani vitakuwa havina tena thamani.

Post a Comment

Previous Post Next Post