Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida amesema yeye hayumo kwenye kambi yoyote ya wanaharakati
wanaowania urais ndani ya CCM na kusisitiza kuwa kambi yake ni moja tu
CCM.
Madabida aliitoa kauli hiyo wakati alipokuwa
akitoa shukrani kwa wananchi wa Mtaa wa Kijichi kwa kukipa kura chama
cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji
2014.
“Madai hayo siyo ya kweli, mimi sipo katika kambi
yoyote, kambi yangu moja tu Chama cha Mapinduzi.” Madabida ameyasema
hayo muda mfupi baada ya kuwashukuru wananchi hao wa mtaa wa kijichi kwa
kukipa kula chama cha CCM kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtaa huo, Ramadhan
Kiula.
Akizungumza na wananchi hao, Madabida alisema nchi
yetu inachangamoto nyingi ikiwamo za kiuchumi, kisiasa na kijamii na
kwamba CCM inajitahidi kukabiliana nazo hivyo aliwataka wananchi
wasifanye wasifanye makosa katika uchaguzi ujao kwa sababu sumu
haionjwi.
Madabida amesema kuhusu Katiba inayopendekezwa
mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa lakini ni kweli ajenda yake ni
ya CCM ambayo ipo madarakani, siyo ya wapinzani ila Katiba siyo ya CCM
ni ya wananchi.
“Rasimu ya pili ya Katiba haikuwa Msahafu ama
Biblia, ndiyo maanda kulikuwepo na bunge maalum la Katiba ambapo lengo
lilikuwa ni kuijadili, kuichambua na inapobidi kubadilishwa na lilifanya
hivyo kwa kufanya mabadiliko ya maboresho katika mambo mapya kwa
asilimia 15 kati ya 100.”Alisema Madabida.
Kuhusu uchaguzi wa uchaguzi wa serikali za Mitaa,
kijiji na kitongoji 2014, Madabida alikiri kuwa kulikuwepo na ushindani
mkubwa na akaongeza kuwa kuna mambo mengi wamejifunza ambayo
yatatusaidia katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk
Faustine Ngugulile aliwataka wananchi hao kuisoma katika inayopendekezwa
kwa kina na katiba ya zamani ili waweze kufahamu wanapiga kura ya nini.
Dk Ndugulile alisema wao kama CCM wanasema Katiba
hiyo inayopendekezwa inatosha na kuwataka wananchi wasije kurubuniwa
ifikapo Aprili 30,2015 wajitokeze kuipigia kura.
Pia aliwataka wananchi kujitokeza katika
kujiandikisha kwa kuwa wasipofanya hivyo kula ya maoni n ahata uchaguzi
mkuu hawatashiriki kwa sababu vitambulisho vya vya zamani vitakuwa
havina tena thamani.
إرسال تعليق