Dar es salaam, Siku tatu baada ya ajali ya moto
kutokea katika eneo la Kipunguni A jijini Dar es Salaam na kusababisha
vifo vya watu sita na nyumba kuteketeatu, Jeshi la Zimamoto limejitete
kuwa lilishindwa kufika haraka kwenye tukio kwa sababu ya ubovu wa
mawasiliano kati yao na wananchi.
Katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni mtoto
katika familia hiyo ndiye aliyenusurika kwani alikuwa matembezini ambapo
aliporudi alikuta moto umeshaanza kuwaka na baadhi ya vitu vilishaanza
kuteketea.
Inspekta wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayaimis
ameeleza kuwa wananchi wasiwalaumu kwa sababu taarifa zilichelewa kufika
ofisini kwao na kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa mabovu.
Amesema alipokuwa anatoka kuelekea eneo la tukio
walipotea njia na kuelekea hadi Kituo cha Polisi cha Sitaki Shari na
badae wasamaria wema waliwaelekeza hadi eneo la tukio.
“Katika nyumba hiyo hakikuwezwa kuokolewa hata
kitu kimoja kwasababu vitu vyote vilishaanza kushika moto na zima moto
walipofika eneo la tukio waliweza kumalizia kuuzima na kutoa miili ya
marehemu na kukabidhi kwa Jeshi la Polisi,”amesema Nzalayaimisi
Ameongezea kwa sasa jeshi hilo linakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa magari , mawasiliano mabovu na
kutojua mitaa mingi ya jijini Dar es Salaam.
Aliwashauri wananchi kutoa taarifa kamili na watu wanapojenga nyumba wahakikishe wanakuwa na milango na madirisha ya dharula.
إرسال تعليق