Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal
kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika
kwa asilimia 99.8.
Mzani wa
Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa
haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya
sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib
Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya
kuukagua.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib
Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa
Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara
ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa
Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya
kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani
walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba
zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Mbunge wa
Chalinze Ridhiwani Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha ngoma
cha Msoga kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye urefu
wa km 10. Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika eneo la
Chalinze.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib
Bilal akisalimiana na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua Mzani
wa Vigwaza.
Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu ambaye
pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi wa
Mzani wa Vigwaza.
Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli wakielekea kwenda kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt.
Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha
zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya
Ujenzi
Post a Comment