Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake Sanura Kassim.Habari rasmi kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba, mama mzazi wa Diamond amerejea nchini wikiendi iliyopita huku hali yake ikionekana kuimarika vizuri tofauti na mwanzo ambapo alirejeshwa nchini akiwa hoi kufuatia kushambuliwa na ugonjwa wa kupooza mkono na mguu.
“Kwa taarifa yenu mama Diamond amerudi yupo nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar).
“Cha msingi anamshukuru Mungu kurejea kwa afya yake ambapo kwa sasa yupo fiti, kaondokana na tatizo la kupooza, kwa sasa anaweza kutembea na kushika chochote kwenye mkono.
“Nimefurahi
sana kumuona kwenye hali hiyo maana sasa hata unapoongea naye mwenyewe
unajisikia faraja kwani ana amani moyoni mwake, ingawa bado anamalizia
kutumia dozi na mara kadhaa dawa anazokunywa zinamfanya kupitiwa na
usingizi sana, ila kwa hali yake sasa hakuna ubishi tena amepona na
familia ina amani kwa jumla,” kilisema chanzo chetu kinachomtembelea
mama Diamond nyumbani mara kwa mara.Jirani wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake kuandikwa alisema kitendo cha mama Diamond kurejea akiwa na afya njema kimemfurahisha sana.
إرسال تعليق