Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akimkaribisha Ikulu Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella
Schadt wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam tarehe
3.2.2015.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Ujerumani Mama Daniella Schadt akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova kwenye viwanja vya Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la
Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea
salamu ya heshima mara baada ya mgeni huyo kuwasili Ikulu akiwa kwenye
ziara ya kiserikali hapa nchini.
Rais Jakaya Kikwete na Mke wake
Mama Salma wakiandamana na wageni wao Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Bwana
Joachim Gauck na Mke wake Schadt wakingia Ikulu huku mamia ya wananchi
wakishangilia kwa furaha huku wakipeperusha bendera za hizo nchi mbili.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt Ikulu.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Ujerumani Mama Daniella Schadt akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, wakati mgeni huyo alipowasili
kwenye ofisi hizo akiambatana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,
Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Daniella
Schadt wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya WAMA, Mama Hulda
Kibacha (kushoto ni Blandina Nyoni (kulia) wakati mgeni huyo
alipotembelea ofisi hiyo
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Ujerumani Mama Daniella Schadt akiweka saini yake kwenye kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za WAMA akiambatana na
mwenyeji wake Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akikabidhi Jarida la WAMA kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama
Schadt wakati alipotembelea ofisi za WAMA.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Schadt zawadi ya kanga.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akifanya mazungumzo na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani
Mama Daniella Schadt kwenye ofisi za WAMA tarehe
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Ujerumani Mama Schadt akiagana na wajumbe wa bodi ya WAMA pamoja na
wafanyakazi mara baada ya kutembelea ofisi hizo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiambatana na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama
Daniella Scahdt wakimwangalia mgonjwa Kundi Girogui aliyetoka wilaya ya
Serengeti ambaye aliyefanyiwa upasuaji wa mdomo kwenye hospitali ya
CCBRT huko Msasani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiagana na mgeni wake Mama Daniella Schadt, Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Ujerumani mara baada ya viongozi hao kutembelea hospitali ya CCBRT huko
Msasani
Post a Comment