Walimu wageuka wazazi Shule ya Msingi Mapambano

Shule ya Msingi Mapambano imetimiza miaka 35 tangu ilipoanza, ikiwa na wanafunzi 150 na walimu watano. Kwa sasa ina wanafunzi 403 na walimu 22.
Kimatokeo shule hii ina historia ya kuridhisha ya wanafunzi wake kufanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kwa miaka miwili (2013 na 2014), wanafunzi 138 walifaulu kati ya 141.
Hata hivyo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Amina Msangi anasema pamoja na mafanikio yaliyojitokeza, ugumu wa maisha kwa baadhi ya familia unawakwaza watoto kujifunza kwa ufanisi.
“Unaweza kumrudisha nyumbani mara tatu mwanafunzi kwa tatizo dogo, lakini mzazi anashindwa kumsaidia hivyo unagundua kuwa ni hali ya maisha tu,” anasema na kuongeza:
“Kwa mfano, mtoto anakosa kiatu, mkanda hata nauli ya daladala kurudi nyumbani, lakini kwa kutambua umuhimu wa masomo yao inabidi kujitoa...Tumeamua kuzifanyia kazi changamoto hizo.”
Changamoto nyingine anataja kuwa ni kukosekana kwa uzio shuleni hapo, jambo linalosababisha watu wa nje kuingia na kutumia huduma za vyoo.
“Hata wakati mwingine usalama unakua kidogo kwa wanafunzi wetu,” anasema

Post a Comment

Previous Post Next Post