Shule ya Msingi Mapambano imetimiza miaka 35 tangu ilipoanza,
ikiwa na wanafunzi 150 na walimu watano. Kwa sasa ina wanafunzi 403 na
walimu 22.
Kimatokeo shule hii ina historia ya kuridhisha ya
wanafunzi wake kufanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi. Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kwa miaka miwili (2013 na 2014),
wanafunzi 138 walifaulu kati ya 141.
Hata hivyo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Amina
Msangi anasema pamoja na mafanikio yaliyojitokeza, ugumu wa maisha kwa
baadhi ya familia unawakwaza watoto kujifunza kwa ufanisi.
“Unaweza kumrudisha nyumbani mara tatu mwanafunzi
kwa tatizo dogo, lakini mzazi anashindwa kumsaidia hivyo unagundua kuwa
ni hali ya maisha tu,” anasema na kuongeza:
“Kwa mfano, mtoto anakosa kiatu, mkanda hata nauli
ya daladala kurudi nyumbani, lakini kwa kutambua umuhimu wa masomo yao
inabidi kujitoa...Tumeamua kuzifanyia kazi changamoto hizo.”
Changamoto nyingine anataja kuwa ni kukosekana kwa
uzio shuleni hapo, jambo linalosababisha watu wa nje kuingia na kutumia
huduma za vyoo.
“Hata wakati mwingine usalama unakua kidogo kwa wanafunzi wetu,” anasema
إرسال تعليق