Moto
Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa
Jamuhuri na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa
kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa
kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa
mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado
hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha
amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea
kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja
wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea
kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo
hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Jamuhuri na moski.
Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.
إرسال تعليق