Maduka ya wafanyabiashara mbali mbali yaliyopo mtaa wa india jijini
Tanga yameteketea kwa moto kwa kile kinachodaiwa kuwa imetokana na
hitilafu ya umeme.
Moto huo uliokuwa ukifukuta ndani katika maeneo hayo ya biashara
ulisababisha baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo kutaka kulishambulia gari
la zima moto la halmshauri ya jiji la Tanga kufuatia kufika katika eneo
la tukio lakini wakati linaaza zoezi hilo ghafla likaishiwa na maji
katika kipindi cha dk 3 na kuamsha hasira kwa mamia ya wananchi.
Hata hivyo akielezea hatua hiyo kamanda wa opesheni wa kikosi cha
zima moto mkoani tanga Bwana Kumenya Bakari amekemea vikali jazba za
wananchi za kushambulia mara kwa mara gari la zima moto la halmashauri
ya jiji la tanga na kufafanua kuwa wanapofika katika eneo la tukio
jambo la kwanza wanaanza kwanaza kuokoa maisha ya watu,mali ndio kisha
baadae kuzima moto katika eneo husika.
- ITV
.jpg)
Post a Comment