Wakati vitendo vya utekaji na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
vikiwa vimekithiri wananchi wa vijiji vilivyopo katika kata ya
oldonyosambu wilayani arumeru wameafikiana kuunda kamati za walemavu
ndani ya vijiji vyao zitakazokuwa na jukumu la kuwatambua walemavu wote
waliopo kama njia mojawapo ya kuwalinda na kuhakikisha upatikanaji wa
haki zao.
Mpango wa uundwaji wa kamati hizo unaratibiwa na asasi moja isiyo
ya kiraia iitwayo HACRET inayoshughulikia maendeleo ya watoto na watu
wenye ulemavu katika mikoa ya arusha na manyara,hatua ambayo viongozi wa
vijiji hivyo wanasema itasaidia kuwatambua watu wao hata pale
wanapopatwa na matatizo..bw paul naikara-M/KITI kijiji cha lemambe.
Akizungumzia vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu
wa ngozi,mkurugenzi wa asasi hiyo LOY YAMAT anasema serikali inapaswa
kuchukua hatua za makusudi kukomesha vitendo hivyo ambavyo licha ya
kupoteza maisha ya binadamu wasio na hatia lakini pia vinalidhalilisha
taifa huku baadhi ya wananchi wakishauri kutafutwa na kuwekwa wazi
waganga wote wanaohamasisha vitendo vya ushirikina.
Wananchi hao pia wameshauri mashirika na watu binafsi wenye uwezo
kujenga utamaduni wa kuwasaidia walemavu na ikibidi kuwajengea mazingira
ya kujiendeleza kiuchumi wakimtolea mfano mwenyekiti wa makampuni ya
IPP Dakta.Reginald Mengi.
- ITV

Post a Comment