Wananchi oldonyosambu waunda kamati za vijiji kulinda watu wenye ulemavu

Wakati vitendo vya utekaji na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi vikiwa vimekithiri wananchi wa vijiji vilivyopo katika kata ya oldonyosambu wilayani arumeru wameafikiana kuunda  kamati za walemavu ndani ya vijiji vyao zitakazokuwa na jukumu la kuwatambua walemavu wote waliopo kama njia mojawapo ya kuwalinda na kuhakikisha upatikanaji wa haki zao.
Mpango wa uundwaji wa kamati hizo  unaratibiwa na asasi moja isiyo ya kiraia iitwayo HACRET inayoshughulikia maendeleo ya watoto na watu wenye ulemavu katika mikoa ya arusha na manyara,hatua ambayo viongozi wa vijiji hivyo wanasema itasaidia kuwatambua watu wao hata  pale wanapopatwa na matatizo..bw paul naikara-M/KITI kijiji cha lemambe.
 
Akizungumzia vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi,mkurugenzi wa asasi hiyo LOY YAMAT anasema serikali inapaswa kuchukua hatua za makusudi kukomesha vitendo hivyo ambavyo licha ya kupoteza maisha ya binadamu wasio na hatia lakini pia vinalidhalilisha taifa huku baadhi ya wananchi wakishauri kutafutwa na kuwekwa wazi waganga wote wanaohamasisha vitendo vya ushirikina.
 
Wananchi hao pia wameshauri mashirika na watu binafsi wenye uwezo kujenga utamaduni wa kuwasaidia walemavu na ikibidi kuwajengea mazingira ya kujiendeleza kiuchumi wakimtolea mfano mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dakta.Reginald Mengi.
- ITV

Post a Comment

أحدث أقدم