MOURINHO AMALIZA MGOMO BARIDI NA VYOMBO VYA HABARI - Aishambulia Man City kwa matumizi ya fujo

Jose Mourinho amevunja ukimya wake kwa vyombo vya habari na hapo hapo akaishambulia Manchester City kwa kukiuka taratibu za manunuzi (financial fair play rules - FFP).
Mourinho alikuwa kwenye mgomo baridi wa kuzungumza na vyombo vya habari tangu lilipotokea sakata la kufungiwa kwa mshambuliaji wake Diego Costa kwa kumsigina mguuni Emre Can wa Liverpool kwenye mchezo wa nusu fainali ya Capital One Cup.
Kocha huyo wa Chelsea akapigwa faini na FA kwa shutuma zake zilizopitiliza dhidi ya waamuzi.
Lakini Ijumaa Mourinho akaibuka na kusema: “Kitu pekee ambacho si kizuri ni kwamba unachuana na timu ambayo haifuati kanuni za FFP.
“Sidhani kama timu inaweza kuwa bingwa huku ikiwa imeadhibiwa, lakini hilo lilishatokea kabla”.
 City imemsajili Wilfried Bony kwa pauni milioni 28 wakati Chelsea ikitumia pauni milioni 7 licha ya kumnunua Juan Cuadrado kwa pauni milioni 27.

Post a Comment

Previous Post Next Post