Mvua yashughulika na wanakigoma,vikilowa lazima vianikwe

Baadhi ya wafanyabiashara w maduka katika soko kuu la mjini Kigoma wakiwa wametoa nje ya maduka yao bidhaa mbalimbali kutoka katika maduka hayo kufuatia kuathiriwa na maji baada ya mvua kubwa iliyonyesha mjini Kigoma kuingia ndani ya maduka yao.




Daraja la posta lililopo karibu na stesheni ya treni ya Mjini Kigoma likiwa limesombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa takriban masaa mawili na nusu na kuleta uharibifu wa miundo mbinu na kubomoa nyumba mbalimbali za wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji.

Post a Comment

أحدث أقدم