Mfalme Mzee Yusuf akiimba na mashabiki wimbo wake mpya wa Mahaba Niue.
Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa My Valentine.
Muimbaji wa Jahazi, Leila akiimba Wimbo wa Fanya Yako.
Khadija Yusuf naye akiimba na mashabiki wimbo wake wa Hasidi Hana Sababu.
Mwansiti Mbwana akiwakonga na Wimbo wa Alipangalo Jalali.
Waimbaji wa Jahazi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki wakimzunguka bi'dada (jina lake halikujulikana) akiyakata mauno.
Umati wa mashabiki wakipagawa na Jahazi Modern Taarab.
KUNDI linalotikisa kunako
miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf
leo limefunika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live katika
shoo maalum ya Usiku wa Wapendanao 'Valentine's Day'.
Jahazi walianza kutawala jukwaa ambapo,
Leila alikuwa wa kwanza kupanda na kuimba Wimbo wa Fanya Yako kisha
akafuatiwa na Mwansiti na Fatuma Nyoro. Baadaye alipanda Mzee Yusuf kwa
Wimbo wa My Valentine na kufanya ukumbi wote kulipuka kwa shangwe. Mzee
Yusuf aliamsha shangwe zaidi baada ya kuimba Wimbo mpya wa Mahaba Niue.
Post a Comment