NDOA iliyodumu kwa miaka miwili na nusu kati ya mwigizaji wa filamu
Jacqueline Pentzel na Gadna Dibibi imevunjika, Ijumaa lina mkanda
kamili.
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao waliachana baada ya kutuhumiana
kutoka nje ya ndoa yao, jambo ambalo baada ya kuvumiliana kwa muda
mrefu, hatimaye wameamua kubwaga manyanga.
Inadaiwa kwamba kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita, mume alikuwa
ameshahama nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri walikokuwa wakiishi na
kuhamia Ilala na Kijitonyama kwa ndugu zake.Baada ya taarifa hizo,
gazeti hili liliwasiliana na Gadna ambaye alisema:
“Ni kweli tuna wiki kama mbili tatu hatupo pamoja, kuna mambo
tumeshindwana, na kweli nimemwandikia talaka na kila mmoja sasa anaishi
kimpango wake,” alisema Gadna.
Jacqueline Pentzel na Gadna Dibibi siku ya ndoa yao.
Naye Jack alipopatikana alikiri kutokea kwa jambo hilo na kwamba talaka
yake imeshaandikwa, isipokuwa bado hajaenda kuifuata Kijitonyama kwa
ndugu wa aliyekuwa mumewe.Licha ya kudaiwa kuwa ishu ya uchepukaji ndiyo
sababu, hakuna aliyekuwa tayari kufunguka juu ya hilo
Post a Comment